• Breaking News

    About us

    • Hii ni shule binafsi ya bweni inayomilikiwa na mtanzania mwenye nia na mapenzi ya dhati kutoa huduma kwa jamii hasa kuinua mwamko wa elimu kwa wazawa katika viwango vya kimataifa.
    • shule inaandikisha na kupokea wanafunzi wa jinsia zote,kabila na dini zote.
    • ila mwanafunzi atalelewa na kukuzwa katika misingi na maadili ya kanisa takatifu katoliki.
    • wanafunzi wote watasoma bweni hakuna kutwa.
      KAULI MBIU YA SHULE
    "SALA,NIDHAMU na KAZI" 
    Mtazamo na msimamo wa shule
    kumuandaa mwanafunzi kujifunza na kufikia upeo kimani,kimaadili,kimaumbile na kitaaluma katika maisha ya familia na kujitoa.shule itahakikisha mwanafunzi anapata haiba yakuwa mwema na kuweza kutumia mafunzo na kueneza ujuzi aliopata kwa familia,jamii,taifana dunia kwa ujumla.

    MALENGO MAHUSUSI YA SHULE
    • Kumuwezesha mwanafunzi kuthamini,kuelewa na kutambua kuwa MUNGU ndiye mpaji na mtoaji wa kila utashi,busara uweza na mawazo yote ya taaluma duniani.
    • kuiendeleza na kuifanya shule kufikia kiwango bora na ngazi ya juu kitaifa na kimataifa
    • kumuandaa mwanafunzi kuwa raia mwema na mwenye kuaminika na kutegemewa kutoka ngazi ya familia,jamii hadi taifa.
    • kutoa elimu bila ubaguzi wa jinsia ,kabila,rangi,wala dini kwa raia wote watakaokidhi vigezo,miongozo na taratibu za shule

      MSISITIZO KITAALUMA
    • Kuwawezesha wanafunzi kuongea kiingereza fasaha na kuwa na uwezo wa kuandika na kusikia lugha hii ya kimataifa na muhimu.
    • kuweka mkazo thabiti na uhamasishaji wa masomo ya sayansi toka vidato vya awali hadi mwisho wa masomo ili kuendana na ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
    • kuwajenga wanafunzi kuweza kujiamini na kuweza kufanya maamuzi sahihi,kwa muda na wakati sahihi kwa njia ya ushauri nasaha na maelekezo ya kitaaluma kwa kutumia mifano hai.
    • kila mwanafunzi atapewa mwongozo na ushauri juu ya kipaji alichonacho katika masomo,michezo na sanaa na wengine kufundishwa kwa mujibu wa uwezo wao.
    • mfumo wa malezi ni "ZUIZI"(preventive) kwa maana kila mahali mwanafunzi atakapokuwepo na mlezi atakuwepo kuanzia bwenini,darasani,kazini,michezoni ili kuhakikisha utashi sahihi unalindwa na asiwepo wa kuharibiwa.
          MTAALA
    Shule inafuata mtaala wa tanzania 2-7-4-2-3 na kumwezesha mwanafunzi kupata cheti cha kidato cha nne toka baraza la mitihani tanzania (NECTA) Kwa daraja la (CSEE)
    Masomo ya dini maadili,sayansi na sanaa yanatolewa shuleni.

    MAISHA YA IMANI NA JAMII
    • Sara na hofu ya mungu ndio muongozo wa kila mwanafunzi,mwalimu na mfanyakazi kwa kila afanyacho nje na ndani ya shule.
    • kila mwanafunzi atapewa mwongozo na ushauri juu ya ya kipaji alichonacho katika masomo,michezo na sanaa na wengine kufundishwa kwa mujibu wa uwezo wao.

    1 comment:

    1. Tunaomba pia mtuwekee na bank details. Nachanganuo wa ada

      ReplyDelete